Showing posts with label siasa. Show all posts
Showing posts with label siasa. Show all posts

Sunday, 19 April 2015

NEC: UCHAGUZI MKUU HAUTASOGEZWA MBELE

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema kuwa, Uchaguzi Mkuu utafanyika kama ulivyopangwa na haiwezi kusegeza mbele tarehe ya uchaguzi huo kutokana na suala hilo kuwa ni la kikatiba.

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Mstaafu Damian Lubuva akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Manunuzi na Logistic, Gregory Kaijage na kushoto ni Naibu Katibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Mkuu wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama), Sisti Chriati.

 Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Mstaafu Damian Lubuva amesema kuwa wanasiasa wamekuwa na kauli ambazo zinawafanya wananchi wapate hofu wakati suala hilo kuhairisha uchaguzi halipo katika tume.
Baadhi ya Wandishi wa habari waliohudhuria katika mkutano wa habari wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi jijini Dar es Salaam.
jaji Lubuva ameongeza kuwa wanasiasa wanatakiwa kuangalia maneno ambayo wanayatoa kwani hayana msingi, wanatakiwa watoe sera zao za vyama kwa wananchi na sio kuisemea tume mambo ambayo hayana ukweli wowote.

Wednesday, 15 April 2015

ZITTO: Msimamo wa ACT Wazalendo kuhusu Ushirikiano wa vyama


Kumekuwa na shauku ya wananchi kwa sisi kushirikiana na vyama vingine vya siasa ili kufanikisha malengo yetu ya kuleta mapinduzi ya kiuchumi kwa kuubomoa mfumo wa uchumi unaonyonya wananchi. Msimamo wetu upo wazi na tumeueleza mara kadhaa.



1 tunaunga mkono juhudi zozote za kushirikiana kwa vyama na hili linathibitishwa na jina letu ALLIANCE na Msimamo wetu kuhusu mabadiliko ya Katiba.

2 tunataka ushirikiano utakaonufaisha wananchi na sio ushirikiano wa kugawana nafasi za uongozi.

3 hatuna shida na Tupo tayari kushirikiana na chama chochote kilicho tayari kushirikiana na sisi ikiwemo UKAWA ili kuunganisha nguvu kuitoa CCM kwa malengo ya kujenga uchumi shirikishi wenye kuzalisha ajira nyingi na bora, wenye mfumo wa hifadhi ya jamii kwa wananchi wote na wenye kutokomeza umasikini.

Monday, 13 April 2015

Kiongozi wa DA kutogombea uchaguzi ujao

Kiongozi wa chama cha upinzani nchini Afrika Kusini cha Democratic Alliance,DA, amesema hatagombea katika uchaguzi wa chama hicho mwezi ujao.
Helen Zille kiongozi wa chama cha Democratic Alliance cha nchini Afrika Kusini

Helen Zille amesema ni wakati muafaka kwake kutogombea, akisema kuwa DA watanufaika na mchango wa vijana. Atabaki kuwa waziri mkuu wa jimbo la Western Cape hadi mwaka 2019.
Bi Zille, mwandishi wa habari wa zamani na mwanaharakati wa kupinga ubaguzi wa rangi amekiongoza chama hicho tangu mwaka 2007.

Sunday, 12 April 2015

Umoja wa Wanavyuo Vikuu Iringa Wamuomba EDWARD LOWASSA kugombea URAIS 2015


Wanavyuo hao wapatao 1500 walioungana toka vyuo vikuu na vyuo vya kijamii Iringa wamesema kuwa wanamuomba Lowasa agombee uraisi na wako tayari kumuunga mkono. Wameyasema hayo wakiongea na waandishi wa habari wakati wakijitolea damu na kufanya usafi ktk hospitali ya rufaa ya mkoa wa Iringa.

Source: ITV habari

Friday, 10 April 2015

Zitto Kabwe Aanza Vizuri ACT Wazalendo, Afanya Mkutano wa Kwanza Songea, Watu Wafurika Kumsikiliza.

Picha Kiongozi wa ACT Wazalendo Ndugu Zitto Z.Kabwe akihutubia umati mkubwa wa wana Songea waliohudhuria kumsikiliza,ikiwa ni ziara yake ya kwanza toka ang'atuke katika chama cha CHADEMA.
Shilole bado ana nia ya kugombea ubunge kwenye jimbo lake la Igunga, lakini anahofia kuwa maisha yake yanaweza kuwa hatarini!

Shilole ameiambia Bongo5 kuwa amepokea simu nyingi kutoka Igunga zinazomtaka ajitose kuwania nafasi hiyo, lakini bado yupo njia panda.

Unajua siasa ni ngumu mimi bado nipo kwenye mjadala wa kugombea na hii ni baada ya kuona watu wanataka kuongozwa, lakini bado nafikiria,” amesema. “Nikiwa tayari nitagombea kupitia CCM. Kitu ambacho kinaniogopesha kiukweli ukiangaliwa watu waliopita ni vijana tu wanakufa mapema kutokana na mambo ya siasa. Siasa inahitaji moyo sana mimi ni muoga sana, naogopa kufa watu wanauwana! Mtu unatamani lakini ndo hivyo,” ameongeza.

TANESCO Yatangaza Mgawo wa Umeme wa Siku Tisa Kutokana na Upungufu wa Nishati hiyo Katika Gridi ya Taifa

Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) limetangaza mgawo wa umeme kwa siku tisa katika baadhi ya maeneo kutokana na upungufu wa nishati hiyo katika Gridi ya Taifa.

Hali hiyo imetokana na maombi ya Kampuni ya Pan African Energy (PAT) inayosimamia uzalishaji wa gesi asilia Songosongo kusimamisha uzalishaji kwa nyakati tofauti ili kufanya matengenezo na kubadilisha baadhi ya vifaa kwenye mitambo yake.



Taarifa ya shirika hilo kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana ilisema shughuli hiyo itafanyika kwa siku tofauti kati ya Aprili 6 na Mei 10.