Wakurugenzi na viongozi mbalimbali wa
Radio za jamii wamethibitisha kupokea na kuanza kurusha Katiba
Inayopendekezwa kwa njia ya sauti, makala na michezo ya radio
iliyoandaliwa na Kampuni ya Focus Media na COMNETA zenye maudhui ya
katiba inayopendekezwa.
 |
| Wasimamizi
wa redio za jamii wakisikiliza kwa makini wakati wa mafunzo ya
kuwajengea uwezo yaliyofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam. |
Wakizungumza na Focus Media ambao ndio waandaaji na
wasambazaji wamekiri kwamba wamepokea kwa wakati muafaka, kwani hawakuwa
na chanzo sahihi cha kupata maudhui yanayohusu elimu ya uraia na
uchaguzi mkuu na kura ya maoni.

 |
| Mwenyekiti
wa Mtandao wa redio za Jamii, Joseph Sekiku akiongea machache kabla ya
kuwagawia wasimamizi wa redio za jamii wakati wa mafunzo ya kuwajengea
uwezo yaliyofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam. |
Baadhi ya wasimamizi wa radio zilizo katika mtandao wa radio
za kijamii Community Media Network of Tanzania ambao wamethibitisha
kupokea vitendea kazi hivyo ni Bw. Ali Khamis Mtwana, Mkurugenzi
Mtendaji wa Tumbatu Island Community Radio, Bw. Anton Masai Triple A FM
Arusha, Dr. Lazaro Ole Mongoi Mkurugenzi Mtendaji wa IDEA Radio, Henry
Bernard, Adelina Lweramla, Jackson Mollel, wa ORS FM Arusha, Edwin
Mpokasye, Radio Fadhila Mkurugenzi Radio Kwizera- Ngara.
Mkurugenzi
Mkaazi wa UNESCO nchini Tanzania Bi Zulmira Rodrigez, akiwagawia
wasimamizi wa redio za jamii katiba iliyopendekezwa iliwekwa kwa nji ya
sauti.
No comments:
Post a Comment