KESI YA KUDAIWA DENI: D’BANJ AKACHA MAHAKAMA, MDAI NAYE HAKUFIKA
Mwanamuziki maarufu wa Nigeria anayejiita ‘Eja
Nla’ (Samaki Mkubwa) ambaye jina lake halisi ni , Dapo Oyebanjo,
akijulikana pia kama D’Banj, hakufika mahakamani wakati wa kuanza kwa
kesi ambayo anashitakiwa kwa kutolipa deni.
 |
| Dapo Oyebanjo 'D’Banj' |
Kesi hiyo ilikuwa ianze kuunguruma Machi 30 mwaka huu kwenye mahakama
ya Multi-Door Courthouse, eneo la Obalende, Lagos,lakini mwanamuziki
huyo hakufika. Mlalamikaji , Henry Ojogho, naye hakufika.
Hata hivyo, wakili wake (D’Banj) aitwaye Dele Adeshina, alifika mahakamani.
Wakati huohuo, hakimu aliyepangwa kusikiliza kesi hiyo, Bi Oyebanji,
aliiahirisha hadi Mei 7 mwaka huu itakaposikilizwa tena.Ojogho, ambaye
ni Naibu Mwenyekiti wa kampuni la Broron Group and MindHub
Technologies, alidai kwamba D’Banj ambaye ndiye mmiliki wa kampuni la
DB Records, alimkopa Naira milioni 60 lakini akakataa kuzilipa kama
alivyoahidi.
No comments:
Post a Comment