| Polisi wakiwa wamefunga barabara baada ya tukio la mauaji |
Polisi hawajamtambua muuaji lakini afisa mmoja ambaye hakutaka jina lake litajwe ameviambia vyombo vya habari nchini Marekani kuwa jina lake ni Chris Harper Mercer.
Sababu za muuaji huyo kutekeleza shambulio hazijajulikana, ingawa Polisi wanasema wanafanyia uchunguzi ripoti kuwa alitahadharisha dhamira yake katika mtandao wa kijamii.
Saa kadhaa baada ya shambulio, ambalo watu saba walijeruhiwa Rais wa Marekani, Barack Obama ametaka kuwe na sheria kali za udhibiti wa silaha.
No comments:
Post a Comment