| Jenerali Diendere |
Jenerali Gilbert Diendere ,kiongozi
wa mapinduzi ya mwezi uliopita nchini Burkina Faso anazuiliwa na vikosi
vya usalama vya taifa hilo .
Kaimu wa rais Michel Kafando alirudishwa mamlakani wiki iliopita kufuatia kuingilia kati kwa jeshi pamoja na viongozi wa Afrika Magharibi.
| MIchel Kafando |
Jenerali Diendere amewasilishwa kwa mamlaka ya Burkinabe,kulingana na duru za mahakama.
Awali kiongozi huyo alikuwa amekimbilia hifadhi katika afisi ya mwakilishi wa Vatican nchini humo.
Hatahivyo maelezo zaidi ya kusalimu amri bado hayajulikani.
No comments:
Post a Comment