Wednesday, 1 July 2015

UN TANZANIA YAKUSANYA MAONI KUHUSU UTENDAJI WAKE NCHINI

Na Modewji blog team

Shirika la Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania limetoa nafasi ya kipekee kwa watanzania kutoa maoni yao wakati wa kipindi hiki cha maonyesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar-es-salaam, yaliyoanza kurindima Juni 28, huku wakikusanya maoni mbalimbali kutoka kwa wananchi juu ya utendaji wake kwa wanaotembelea kwenye maonyesho hayo kila siku.
Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu akimwelekeza Mkurugenzi wa kampuni ya Events World, Dimo Debwe Mitiki, jinsi ya kuwasilisha maoni yake kuhusiana na kazi za Umoja wa Mataifa na nini angependa Umoja huo ufanye zaidi kwa ajili ya watanzania kwenye viwanja vya maonyesho ya 39 ya biashara ya kimataifa maarufu kama “Sabasaba”.

Aidha, katika kupokea maoni hayo, UN imeweka utaratibu wa moja kwa moja kwa wananchi kufika kwenye banda lao na kutoa maoni yao, ambayo yanaenda moja kwa moja kwa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) Nchini Alvaro Rodriguez.

Njia nyingine ya kuwasilisha maoni ya moja kwa moja ni kupitia mtandao wa (Online) kwa kuingia http://gpl.cc/UN2
Kupitia linki hiyo, mtumiaji anaweza kutumia simu yake ya smartphone, laptop na vifaa vingine vya kielektroniki.
Njia nyingine ni ya kutumia ujumbe mfupi wa maandishi (SMS), ambapo kwa watumiaji wa mtandao wa Airtel watatuma ujumbe wao kwenda namba 15453, kwa watumiaji wa mtandao wa Tigo wanatuma kwenda 15055 au 15453 na kwa Vodacom ni namba 15055.
Na kwa njia ya tatu ni kuwasilisha namba ya simu na majina na ujumbe unaotaka na UN wataufanyia kazi.
Aidha, maoni hayo yatakuwa yakipokelewa kwa kipindi chote cha SabaSaba, hivyo wananachi wameombwa kujitokeza kwa wingi kutoa maoni yao ya nini UN wakifanye nchini pamoja na mambo mengine.

No comments:

Post a Comment