Rais wa Benki Kuu ya Ulaya, Mario Draghi, amesema ameshindwa kuidhinisha fedha zozote bila ya mpango wa dharura wa kuokoa uchumi. Wakopeshaji wa Kimataifa wana kadiria kuwa Ugiriki inaweza kuhitaji hadi euro bilioni themanini na sita ili kuepuka kuanguka kiuchumi.
Mawaziri wa ukanda wa sarafu ya euro wameripotiwa kuanda mipango madhubuti ya mageuzi ambayo yataitaka bunge la Ugiriki kupitisha iwe sheria na wachunguzi wa fedha kutumwa Ugiriki. Mwandishi wa BBC huko Athens anasema Tsipras anaweza kuwapanga upya mawaziri wake wiki hii.
No comments:
Post a Comment