Upangaji wa makundi wa soka ya
wanawake ya Michezo ya Afrika (All Africa Games) itakayofanyika nchini
Congo Brazzaville kuanzia Septemba 4-19 umefanywa na Shirikisho la soka
barani Afrika, CAF na timu ya taifa ya soka ya wanawake ya Tanzania,
Twiga Stars imepangwa Kundi A pamoja na wenyeji Kongo, Nigeria na Ivory
Coast.
Upangaji wa makundi hayo umefanyika leo makao makuu ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) mjini Cairo, Misri. Kundi B lina timu za Cameroon, Afrika Kusini, Ghana na Misri. Upande wa wanaume, Kundi A lina timu za Kongo, Sudan, Zimbabwe na Burkina Faso, wakati Kundi B kuna Ghana, Senegal, Misri na Nigeria.
No comments:
Post a Comment