Viongozi wa kitaifa kutoka nchi za
Ulaya zinazotumia sarafu ya euro wanatarajiwa kuwa na kikao cha dharura
Jumatatu ijayo, baada ya kushindwa kwa jitihada za hivi karibuni za
kutatua mgogoro wa deni la Ugiriki.
Mawaziri wa fedha wa nchi
zinazotumia sarafu ya euro, baada ya mkutano wao nchini Luxembourg,
wamesema hakuna maendeleo yoyote yaliyofikiwa katika suala la madeni na
makataba wa Ugiriki kuhusu madeni hayo.
Ugiriki lazima ilipe deni
lake kubwa kwa Shiriks la Fedha Duniani, IMF, kufikia mwishoni mwa mwezi
huu la sivyo ikabiliwe na uamuzi wa kuitoa katika muungano wa nchi za
Euro.
Waziri wa Fedha wa Ugiriki Yanis Varoufakis amesema
aliwasilisha mipango ya kuinusuru nchi yake isiwe mufilisi, lakini
amesema makubaliano yoyote yatakayofikiwa lazima yahusishe upunguzaji
deni.
No comments:
Post a Comment