Kiongozi wa ujasusi wa Rwanda ameachiliwa kwa dhamana.
Luteni jenerali Karenzi Karake ametakiwa kufika kwenye kituo cha polisi
kila siku. Luteni jenerali Karenzi Karake alikamatwa siku ya jumamosi
katika
uwanja wa ndege wa Heathrow Jumamosi iliyopita chini ya kibali cha
kukamatwa cha ulaya.
KK anatakiwa na Madrid kuhusiana na vifo vya wafanyikazi wahispania
waliokuwa wakihudumia mashirika ya misaada na mauji ya kimbari nchini
Rwanda.
Rwanda imeonyesha masikitiko yake na kukamatwa kwake.Luteni jenerali Karenzi Karake, mwenye umri wa miaka 54 ni mtu wa kwanza
wa ngazi ya juu kutoka kwa orodha ya watu 40 walio na wadhfa mkubwa
katika jeshi la RPF orodha iliyotolewa na jaji mmoja wa Uhispania
akitaka wakamatwe.
No comments:
Post a Comment