Thursday, 25 June 2015

Kiongozi wa ujasusi wa Rwanda ameachiliwa kwa dhamana.

Luteni jenerali Karenzi Karake ametakiwa kufika kwenye kituo cha polisi kila siku. Luteni jenerali Karenzi Karake alikamatwa siku ya jumamosi katika uwanja wa ndege wa Heathrow Jumamosi iliyopita chini ya kibali cha kukamatwa cha ulaya.
KK anatakiwa na Madrid kuhusiana na vifo vya wafanyikazi wahispania waliokuwa wakihudumia mashirika ya misaada na mauji ya kimbari nchini Rwanda.

Rwanda imeonyesha masikitiko yake na kukamatwa kwake.Luteni jenerali Karenzi Karake, mwenye umri wa miaka 54 ni mtu wa kwanza wa ngazi ya juu kutoka kwa orodha ya watu 40 walio na wadhfa mkubwa katika jeshi la RPF orodha iliyotolewa na jaji mmoja wa Uhispania akitaka wakamatwe.

No comments:

Post a Comment