Mamia ya Waumini wamehudhuria ibada
ya mazishi ya watu tisa waliouawa katika kanisa moja lililopo katika mji
Charleston nchini Marekani wiki iliyopita.
Mmoja ya waliouawa alikuwa ni mchungaji Clementa Pinckney. Viongozi wa kanisa wamesema shetani aliingia kanisani hapo siku hiyo ya Jumatano, lakini alishindwa. Waumini nao wametoa maoni yao:Nimeshukuru kuona ibada ni ya kutia moyo, imetia moyo sana na neno alilotoa mchungaji ni mahala pake haswa.
Ni kile ambacho watu wanakihitaji leo, linalotufanya tujue kwamba hata iwe vipi mungu bado yuko katika ufalme wake....''
Imenifanya nihisi kwamba kuna mambo mengi yanaendelea siku hizi katika fikra za watu na kuhisi kwamba kuna ushirikiano na matumaini kwamba tutaungana pamoja kushinda vile ilivyokuwa awali.......
No comments:
Post a Comment