POLISI WAKANUSHA TISHIO LA MAGAIDI KUSHAMBULIA CHUO CHA UHASIBU ARUSHA
KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas,
amekanusha uvumi ulioenea katika mitandao ya jamii kuhusu kukamatwa
magaidi mkoani Arusha usiku wa kuamkia leo waliokuwa wamejitayarisha
kukishambulia Chuo cha Uhasibu (Institute of Accountancy Arusha - IAA)
wakidaiwa kuwa na gari aina ya Toyota Premio nyeusi ikiwa na watu wanne
na bunduki nne aina ya SMG na risasi 160 walipojaribu kuingia chuoni
hapo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Liberatus Sabas
Inadaiwa katika taaifa hiyo isiyojulikana chanzo chake kwamba watu
hao walijifanya ndugu wa mwanafunzi mmoja wa kike anayeishi kwenye
hosteli zilizo ndani ya chuo hicho.
Wanafunzi wa Chuo cha Uhasibu Arusha wakiwa eneo la Old hosteli
Rais wa chuo hicho, Iman Mkumbo, naye amesema habari hizo hazina ukweli wowote.
No comments:
Post a Comment