MADEREVA
wa vyombo mbalimbali vya moto, nchi nzima leo asubuhi wamegoma
kusafirisha abiria ili kuishinikiza serikali kuondoa kero mbalimbali
zinazowakabili ikiwemo ukosefu wa ajira za uhakika pamoja na agizo la
kutaka kwenda kusoma.

Awali kabla ya mgomo wa leo, Katibu wa Muungano wa vyama vya madereva Bw. Rashid Saleh, alisema baadhi ya kero zitakazopelekea mgomo wa leo ni pamoja na suala la kurudia kusoma kila wanapohuisha leseni zao ambayo wanadai ni aina nyingine ya unyanyasaji kwa maelfu ya madereva nchini, ambao kwa kipindi kirefu wamekuwa hawana mfumo mzuri wa ajira licha ya kutupiwa lawama kibao kuwa wao ndio chanzo cha ongezeko la ajali.
| BAADHI YA WASARI WAKITUMIA MAGARI BINAFSI |
Kwa mujibu wa kiongozi huyo wa muungano wa madereva, wamegoma maana wamechoka kudharauliwa hata kwa mambo ya msingi yanayogusa maisha yao.
Baadhi ya dharau alizozitaja ni pamoja na wamiliki wa mabasi (yaani waajiri wao) kuwaita wao ni wahuni ilhali ni watu wazima, wenye familia, wanaofanya kazi halali na wanaohitaji kuheshimiwa.
No comments:
Post a Comment