Nigeria wafanya uchaguzi wa wabunge na magavana leo
Rais mteule wa Nigeria Bw. Muhammadu Buhari.
Wapiga kura nchini Nigeria watapiga kura leo kuchagua magavana wa majimbo pamoja na wabunge.
Raia wa Nigeria kupiga kura ili kuwachagua wabunge
Chama
cha APC kinatarajiwa kupata ushindi mkubwa baaada ya mgombea wake wa
urais Muhammadu Buhari kumshinda rais Goodluck Jonathan wiki mbili
zilizopita. Hata hivyo chama cha bwana Jonathan cha PDP
kinatarajiwa kupata ushindi kwenye maeneo mawili likiwemo eneo la Lagos
ambalo huchangia theluthi moja ya uchumi wa Nigeria pamoja na jimbo
lenye utajiri wa mafuta la Rivers. Usalama unatarajiwa kuwa wa juu kutokana na hofu ya mashambulizi kutoka kwa kundi la Boko Haram.
No comments:
Post a Comment