Polisi mjini London wamekuwa
wakiupekua msikiti ikiwa ni miongoni mwa uchunguzi wake wa mauaji ya
Imam mmoja wa zamani kutoka Syria.
Msemaji wa polisi amesema kuwa maafisa wamekuwa wakiwasiliana na wawakilishi wa jamii ya waislamu ili kuwahakikishia kwamba upekuzi huo huo ni muhimu, na kwamba msikiti huo utafunguliwa haraka iwezekanavyo.
Abdul Arwani ameripotiwa kuwa mpinzani wa rais Assad wa Syria.
Watu wawili wamekamatwa kuhusiana na mauaji hayo.
No comments:
Post a Comment