Tume ya Taifa ya Uchaguzi Nchini Tanzania
itaanza kusambaza mashine za BVR 248 katika mikoa saba nchni Tanzania
Kuanzia katikati mwa wiki ijayo.
Mikoa iliyopangwa kuanza kupokea mashine
hizi ni mikoa ya Lindi, Mtwara, Ruvuma, Iringa, Wakati zozi likianza
mikoa hiyo nyingine zitakuwa zinapelekwa katika mikoa ya Katavi, Mbeya
na Dodoma. Mikoa mimgine ni Singida Tabora Geita na Kigoma.
Mkuu wa kitengo cha Ufundi wa idara ya
Daftrari/ICT wa NEC Dr Sisit Cariah, Akizungumza na mwandishi wetu
amesema kwamba mpaka sasa wanachi wa mikoa ya Lindi, Mtwara, Ruvumna na
Iringa wakae tayari kwani muda wowote watatangaziwa vituo vya
kujiandikisha.
Pamoja na mshine hizo 248 Tume ya taifa
ya uchaguzi imewaandaa wataalamu 248 ambao watakuwa na jukumu la kutoa
elimu kwa wataalamu wengine 50 kwa kila mmoja nchi nzima kwa ajili ya
kuharakisha uandikishaji kwa mfumo wa BVR.
Dr Sisit Ameeleza kwamba wamefanikiwa
kufanya maboresho makubwa katika mashine hizi ikiwa ni pamoja na
kubadilisha upangaji wa vifaa (settings), mfumo endeshi (Software) na
upande wa Vichapishio (printer) ambazo sasa zimetengenezewa Nchini
Ufaransa umeboreshwa na nirahisi kusafishwa.
Mafunzo yaliyoendeshwa hapa Jijini Dar es Salaam yamechukua siku moja na yamezingatia sana upande wa Vichapishio (printer), Visoma alama za vidole (Finger Print Scaner) na Kamera kutambua macho mekundu. Ameongoza kwamba printer za sasa ni rahisi kusafishwa na hata kuweka kifaa kipya baada ya cha zamamni kuharibika vimerahisishwa.
Kuhusu uchukuaji wa alama za vidole, amesema kwamba kwa sasa tatitzo la mashine ya kuchukua alama za vidole wamelifanikisha kwa asilimia mia. Kwani kwa wale ambao hawana alama za vidole mashine zimewekewa mfumo wa alogarithim mpya ambao uatatambua kila aina ya kidole.
Hata hivyo Kamera zimewekewa mfumo mpya
wa kutambua macho mekundu na kurekebisha rangi ya macho mekundu (Red
eyes) Bila kukwamisha zoezi la uandikishaji.
Mtarajio ni kwamba zoezi lauandikishaji
liwe limekamilika ndani ya kila siku 28 tokea kila mkoa unapopokea
mashine hizi. Vilevile Dr Sisit ameishukuru serekali kwa kufanikisha
upatikanaji wa Vifaa “serekali imejitahidi kuandaa upatikanaji wa
mashine hizo, na usafirishaji kwa njia ya ndege kwenda nchi nzima. Kila
halmashauri na mkoa utachukua angalau siku 28 kukamilisha mkoa utakapo
pokea Vifaa” Dr Sisit amesema.
Mwisho amesema kwamba mashine nyingine 1,600 zitawasili wakati wowote na kwamba serikali imetoa Dola za Marekani milioni 72 (Sh. bilioni 133).
Kuwasili kwa mashine hizo, kunaifanya Nec kupokea mashine 2,098, huku ikisubiri mashine 5,902, ili kukamilisha 8,000 zinazotakiwa. Alisema vifaa hivyo vinanunuliwa na serikali kupitia kampuni ya Lithotech Export ya Afrika Kusini, ambayo imeingia mkataba na Nec na inaviagiza China.

No comments:
Post a Comment