Makundi ya kupigania haki za
kibinadamu yamesema kuwa mikakati ilioafikiwa na muungano wa ulaya
kuzuia idadi kubwa ya wahamiaji wanaojaribu kuvuka hadi Ulaya kutoka
Afrika sio ufumbuzi wa tatizo hilo.
Waandamanaji wakipinga vifo vya wahamiaji wanaovuka bahari ya shamu kwenda Ulaya
Katika kikao cha dharura
kilichofanyika mjini Brussels siku ya alhamisi, Viongozi wa Ulaya
walikubaliana kuongeza msaada wao mara tatu ili kuimarisha usakaji na
uokozi wa wahamiaji katika bahari ya shamu.
Pia waliidhinisha mikakati ya kukamata na kuharibu vyombo vinavyotumiwa kuwasafirisha wahamiaji hao.
Lakini
Shirika la Human Rights Watch pamoja na lile la kuwasaidia watoto la
Save the Children, yanasema kuwa EU inafaa kuongeza juhudi zake katika
uokoaji badala ya kullinda mipaka yake.
Mkutano huo uliitishwa baada ya zaidi ya watu 800 kuuawa wikendi iliopita baada ya boti yao kuzama.
No comments:
Post a Comment