 |
| Rais
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na wachezaji maveterani wa timu
ya Barcelona wakati walimpomtembelea Ikulu jijini Dar es Salaam jana. |
 |
| Mchezaji
nyota wa zamani wa Uholanzi na kocha wa Timu ya maveterani ya Barcelona
Johann Cruyft akimkabidhi jezi Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ikulu
jijini Dar es Salaam jana. |
 |
| Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji
maveterani wa timu ya Barcelona walipomtembelea ikulu jijini Dar es
Salaam jana. |
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho
Kikwete jana, Jumamosi, Aprili 11, 2015, amekutana na wachezaji nyota wa
klabu ya soka la Barcelona ya Hispania katika shughuli iliyofanyika
Ikulu, Dar es Salaam.
Wachezaji hao wakiongozwa na nyota wa Barcelona na timu ya taifa ya
Uholanzi kwenye Fainali za Kombe la Dunia mwaka 1974 nchini Ujerumani
Johann Cruyff pamoja na nyota mwingine wa klabu hiyo na nchi hiyo,
Patrick Kluivert wamekaa Ikulu kiasi cha dakika 40 kabla ya kuondoka
kwenda Uwanja wa Taifa kwa mchezo wao na nyota wa zamani wa Tanzania.
Mheshimiwa Rais Kikwete amewashukuru wachezaji hao kwa kukubali
kutembelea Tanzania na kusema kuwa wanakaribishwa tena kuja nchini kwa
muda mrefu zaidi.
No comments:
Post a Comment