Kiongozi wa chama cha upinzani
nchini Afrika Kusini cha Democratic Alliance,DA, amesema hatagombea
katika uchaguzi wa chama hicho mwezi ujao.
Bi Zille, mwandishi wa habari wa zamani na mwanaharakati wa kupinga ubaguzi wa rangi amekiongoza chama hicho tangu mwaka 2007.
"Uamuzi wa aina hii ulikuwa ni muda mrefu, lakini mwishoni umefanyika ghafla," amesema.
Bi Zille alizaliwa mwaka 1951 kwa Wajerumani wahamiaji. Alikuwa mtetezi wa katiba ya kiliberali ya Afrika Kusini, akiwa mpinzani wa chama kikubwa cha ANC.
Zamani, alimpinga waziwazi Rais Jacob Zuma na aliongoza kampeni ya kutaka afikishwe mahakamani kujibu tuhuma za rushwa.
Bwana Zuma alikana madai hayo, akisisitiza kuwa yeye ni mwaathirika wa "njama za kisiasa".
Chama cha DA kinaungwa mkono zaidi katika jimbo la Western Cape, ambalo lina wakazi wengi weupe na machotara, lakini Bi Zille amejaribu kupenya katika majimbo ya uchaguzi ya waafrika weusi.
No comments:
Post a Comment