Staa mrembo wa Bongo Movies, Aunt
Ezekiel, amesema kwamba anatamani kujifungua, kwani amechoshwa na mimba
yake, kwa sababu imemfanya ashindwe kupata kazi ya kucheza filamu
nyingine.
Akizungumza na gazeti la Mtanzania jana,
msanii huyo alisema kuwa mialiko ya kucheza filamu imekata na sasa
haingizi kipato chochote, badala yake pesa inatoka, hali ambayo
inamfanya atamani ajifungue ili aondokane na adha hiyo.
“Siyo siri nimechoshwa na hii mimba,
natamani hata leo nijifungue, kwani sipati tena tenda za kwenda kuigiza
ambazo huwa zinaniingizia pesa ya kujikimu na sijui lini nitajifungua,” alisema msanii huyo.
Aunt Ezekiel, ambaye aliigiza kama
mhusika mkuu kwenye filamu ya Chozi la Mwanjaa, alisema kwamba anatambua
ujauzito ni baraka na kuna watu wanatamani kupata mimba na hawapati,
lakini wakati mwingine ni kama adhabu

No comments:
Post a Comment