| Ali Kiba na Victoria Kimani. |
| Ben Pol na Wangechi. |
Vee Money na 2 Face (Nigeria)
Vanessa Mdee ‘Vee Money’ anatarajiwa kutinga jukwaa moja na staa kutoka Nigeria, Innocent Ujah Idibia ‘2 Face’ na kukamua nyimbo zao zote kali. Ebu vuta picha 2 Face akiimbishwa Kiswahili ngoma za Vee Money kama vile Me & U na Come Over.
Ben Pol na Wangechi (Kenya)
Staa wa R&B Bongo, Benard Paul ‘Ben Pol’ naye atakuwa ni miongoni mwa mastaa aliyekutana kiulaiiini na kufanya kolabo lake na staa kutoka Kenya, Wangechi. Mashabiki watarajie kumsikia Wangechi akiimba na Ben Pol ngoma kama Ningefanyaje, Jikubali pamoja na Sofia.
Ali Kiba na Victoria Kimani (Nigeria)
Patakuwa hapatoshi pale, mkali wa Bongo Fleva, Ally Saleh ‘Ali Kiba’ atakapopanda na staa wa muziki mwenye asili ya Kenya anayefanya shughuli za muziki nchini Nigeria, Victoria Kimani. Hebu vuta picha pale, Kimani anapokamu na Ali Kiba ngoma kama Chekecha Cheketua pamoja na Mwana.
No comments:
Post a Comment