Kiongozi wa kanisa katoliki duniani
Papa Francis ameripotiwa kukutana na Kim Daviz karani wa Kentucky ambaye
alifungwa jela kwa kukataa kutoa leseni za ndoa za wapenzi wa jinsia
moja,wakati wa ziara yake huko Marekani.
| Kim Davis na Papa Francis |
| Kim Davis |
Alihudumia kifungo cha siku sita mahakamani mapema mwezi huu baada ya kukiuka agizo la mahakama ya kijimbo kutoa leseni hizo kwa wanandoa wa jinsia moja huko Rowan mjini Kentucky.
Mat Stavers,ambaye ndio wakili wa Davis amekiambia chombo cha habari cha CBS kwamba bi Davis na mumewe walikuwa wamealikwa kukutana na papa Francis kufuatia msimamo wake uliotangazwa na vyombo vya habari.
''Papa Francis alimshukuru kwa ujasiri wake na kumwambia aendelee na mwenendo huo'', alisema Bwana Stavers.
No comments:
Post a Comment