Rais mpya wa Nigeria Jenerali Muhammadu Buhari atahudumu pia kama waziri wa mafuta. Msemaji
wa rais Femi Adesina amethibitisha kuwa Jenerali Buhari ambaye katika
miaka 80 alipoiongoza nchi hiyo alishikilia wadhfa wa waziri wa mafuta
atahudumu kama waziri.
 |
|
Rais Muhammad Buhari akihutubia kongamano la viongozi wa dunia huko New York Marekani
|
Hata hivyo naibu waziri ndiye atakayechukua majukumu ya kila siku katika wizara hiyo. Buhari
ambaye aliahidi kupambana dhidi ya rushwa na ubadhirifu wa mali ya umma
inayotokana na mafuta amekuwa nchini Marekani katika kikao cha viongozi
wa dunia cha kongamano la umoja wa mataifa huko New York.
Uchimbaji mafuta unachangia asilimia 70% ya pato la taifa katika
uchumi huo mkubwa zaidi barani Afrika hata hivyo asilimia kubwa ya pesa
hizo huibiwa na kufichwa nje ya nchi.
Jenerali Buhari anatarajiwa kutangaza rasmi baraza la mawaziri wake hii leo. Rais huyo mpya wa Nigeria alichukua hatamu za kuingoza taifa hilo yapata miezi minne iliyopita.
No comments:
Post a Comment