KATIBU wa NEC, Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi, Nape Nnauye
amesema, leo hii majina matano ya makada wa chama hicho walioomba
kuteuliwa na CCM kuwania kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, yatajulikana, na kufuatia majina matatu ya makada hao ambayo
yatapelekwa mbele ya Mkutano Mkuu utakaofanyika Jumamosi Julai 11, 2015.
 |
| Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akizungumza
na waandishi wa habari nje ya Ukumbi wa White House, Mjini Dodoma leo
Julai 10, 2015. |
Nape amesema vikao vyote vinaanza leo saa nne, na hakuna kikao
chochote kilichokwisha fanyika ikiwa ni pamoja na kile kinachozungumzwa
sana na vyombo vya habari yaani kikao cha kamati ya maadili ya chama
hicho ambacho ndicho kinachokata majina na kutoa mapendekezo Kamati Kuu.
Alipoulizwa ucheleweshwaji huo umetokana na nini, Nape alisema "Nyote
mmeshuhudia, Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, amekuwa na kazi
nyingi katika kipindi cha siku mbili hizi na hivyo asingeweza kusimamia
vikao hivyo kama ilivyotarajiwa ingawa amedokeza kuwa "wakubwa" hao
walikuwa wakikutana kwa majadiliano na wadau ingawa hakueleza ni wadau
gani.
No comments:
Post a Comment