Meneja Masoko wa Airtel Money Bwana Stephen Kimea (wa pili kushoto) pamoja na Meneja wa kanda ya Dar es saalam wa Finca Microfinance Benki Bi Sarah Daffer kwa pamoja wakionyesha kipeperushi cha huduma mpya waliyoizundua itakayowawezesha wateja wa Finca kuhamisha pesa kwenye akaunti zao za benki kwenda kwenye akaunti ya Airtel Money, na kuhamisha pesa kutoka Airtel money akanti kwenda akanti ya Finca benki. akishuhudia kushoto ni Meneja Uhusiano wa Airtel Bw Jackson Mmbando, kulia ni Msimamizi wa kitengo cha huduma kwa wateja Finca Vivian Temi.
Meneja
wa kanda ya Dar es saalam wa Finca Microfinance Benki Bi Sarah Daffer
akiongea na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa Ushirikiano kati
ya Finca Micofinance na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel
utakaowawezesha wateja wa benki na Airtel Money kuhamisha pesa kutoka
kwenye akaunti ya benki kwenda kwenye kwenye akaunti ya Airtel Money.na
pia kuhamisha pesa kutoka kwenye akaunti ya AirtelMoney kwenda akaunti
ya benki
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania imesaini makubaliano na benki ya Finca Microfinance yatakayowawezesha wateja wa Benki kuweza kuzifikia pesa zao kirahisi kwa kupitia simu zao za mkononi.Huduma hii mpya itawawezesha wateja wa Airtel kutuma pesa kutoka kwenye akaunti zao za benki kwenda kwenye akaunti zao za Airtel Money na kutoka akaunti zao za Airtel Money kwenda kwenye akaunti zao za benki wakati wowote .Akiongea katika uzinduzi wa huduma hiyo Meneja Uhusiano wa Airtel Bwana Jackson Mmbando alisema “huduma hii inalengo la kuwawezesha wateja wetu kufanya miamala yao mbalimbali ya kifedha wakati wowote kwa usalama Zaidi”.
“Kwa kutambua kuwa Finca sasa ni Taasisi ya Kibenki tumeona ni vyema kuungana nao na kuwawezesha kutoa huduma za kuhamisha pesa zenye usalama na kwa gharama nafuu kupitia simu za mkononi kwa wateja wao nchi nzima”, aliongezaAlisema “ Airtel itaendelea kuboresha huduma zake ili kuweza kufikiamahitaji ya wateja wake kwa kushirikiana na mashirika na Taasisi mbalimbali katika kuboresha huduma zao kwa wateja wao pia”.Kwa upande wake Meneja Masoko wa Airtel Money Bwana Stephen Kimea alisema “ili mteja aweze kufaidika na huduma hii ni lazima awe amejisajili kwenye huduma ya Airtel Money na kuingia kwenye Menu ya Airtel Money ili kutuma pesa kwenda akaunti ya Finca. Kupata Menu Airtel Money mteja atapiga *150*60# na kufata maelekezo. Kuhamisha pesa kutoka akaunti ya Finca kwenda akaunti ya Airtel Money, Mteja ni lazima ajisajili na huduma ya mobile banking na Finca Benki ili aweze kufanya muamala huu. Kuhamisha pesa mteja atapiga *150*19# na kufata maelekezo. Miamala yote ya kuhamisha pesa ni salama na lazima iwe nanamba ya siri ili kukamilika. baada ya muamala kukamilika mteja atapokea ujumbe wa uthibitisho kutoka Airtel Money na Finca benki Akiongea kuhusu huduma hii Meneja wa kanda ya Dar es saalam Finca Microfinance Benki Bi Sarah Daffer alisema” huduma hii itatusaidia sana katika kuongeza ufanisi kwenye huduma zetu katika matawi zaidi ya 26 nchini hivyo tunawashukuru sana Airtel kwa kuungana nasi kupitia huduma za Airtel Money. Tunaamini ushirikiano si utatuwezesha kuongeza idadi ya wateja wetu tu bali utasaidia kuongeza idadi ya miamala inayofanyika kwa urahisi na salama.“Wateja wetu sasa wataweza kufanya miamala ya pesa wakati wowote ,mahali popote mara nyingi zaidi ikiwa tu atajisaliji kwenye huduma hii na akaunti yake ya benki ikiwa hai”, aliongeza aliongezea
No comments:
Post a Comment