Rais Obama ameeleza kuwa anatambua wazi kuwa familia za mateka huwa wanachaganyikiwa pindi wanapo shughulika na serikali yao wenyewe. Ameelezea pia mipango ya baadaye ya serikali yake na sera za nchi hiyo kwamba kutakuwa na utaratibu maalum kiserikali kuratibu jitihada za vitengo mbali mbali na taasisi zingine zinazojitahidi kuwaokoa mateka ambao ni raia wa Marekani.
Ahadi ya Rais Obama kwa raia wake ni kuchukua hatua stahiki kuwarejesha raia wake nyumbani na kuwachukulia hatua watekaji wao.
Ujumbe wangu kwa kila raia wa Marekani ambaye anashikiliwa mateka popote ulimwenguni,ni huu Marekani haitaacha kuhakikisha unaungana na familia yako.hatutasita,hata kama itatuchukua muda mrefu kiasi gani.
No comments:
Post a Comment