| Neymar |
Nyota wa timu ya Brazil Neymar
alionyeshwa kadi nyekundu baada ya kipenga cha mwisho cha mechi ya
kinyang'anyiro cha Copa America baada ya timu yake kufungwa na Colombia
kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1991.
Mshambuliaji huyo wa klabu ya Barcelona alimpiga mpira Pablo Armero kimakusudi kabla ya mchezaji wa Colombia Carlos Bacca pia kupewa kadi nyekundu baada ya kulipiza kisasi kwa kumsukuma Neymar.
Beki Jeison Murillo alifunga bao la pekee baada ya dakka 36.Brazil ilijaribu sana kuimarisha mchezo wake lakini ilishindwa kutengeza nafasi za kufunga goli.
No comments:
Post a Comment