Mpambano
wa Mengi na Manji Wapamba Moto.....Manji Atangaza Kuwa Atajiuzulu yanga
iwapo Aliyosema Mengi yatakuwa ni Kweli..Ataka Mdahalo wa Yeye na Mengi.
Mwenyekiti
wa Yanga, Yusuf Manji amesema atajiuzulu wadhifa wa uenyekiti iwapo
itabainika kuwa kweli yeye ni fisadi, mwizi na muongo kama ambavyo
Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi amekuwa
akisukuma mashambulizi dhidi yake.
Manji amezungumza na waandishi wa habari kwenye makao makuu ya Yanga,
jana na kueleza hayo huku akisisitiza kumtaka Mengi ajitokeze na
wakutane kwa ajili ya kufanya mdahalo wa wazi ambao utadhibitisha
kuhusiana na tuhuma hizo.Alisema kuendelea kuiongoza Yanga wakati imethibitika ni fisadi na mwizi, ni utovu wa nidhamu na wanachama wa klabu hiyo watamtilia shaka.
Manji anadai kilichomchefua zaidi ni habari iliyotoka kwenye Gazeti la Nipashe kuwa kampuni yake ya Farm Equip Tanzania and Quality Garage, ijulikanayo kama QG Engineering ilishindwa kulipa kiasi cha bilioni 9.055 serikalini.
Manji amekanusha taarifa hiyo na kuomba Julai 3, mwaka huu kukutana na mmiliki wa gazeti hilo, Mengi kwenye mdahalo ‘live’ na kila upande uje na ushahidi wa kutosha kisha Watanzania wapige kura ili muongo na mkweli ajulikane kuliko kuchafuliwa jina.
“Iwapo itabainika kweli mimi ni fisadi, muongo na mwizi, niko tayari kuachi ngazi ya uenyekiti wa Yanga na sitagombea cheo chochote hapa, maana klabu itakuwa inaongozwa na mtu asiye na vigezo sitahiki vya kuwa kiongozi,” alisema Manji.
"Watu wanapaswa kujiuliza, mimi ni fisadi ninayejulikana na vyombo vya habari vya IPP tu? Wengine hawaoni hilo? Je, kwa nini IPP pekee ndiyo waone mimi ni fisadi? hapo watu wajiulize," alisema Manji.
No comments:
Post a Comment