Wenyeji wa kombe la Copa America
Chile wamefuzu kufika fainali mara ya kwanza kwa miaka 28. Hii ni baada
ya kuwanyuka Peru mabao mawili kwa moja katika mchuano uliofanyika mjini
Santiago.
Nusura kiungo wa kati wa Chile Arturo Vidal kuondolewa mapema, hata hivyo bahati mbaya ilikua wa mlinda lango wa Peru Carlos Zambrano aliyepewa kadi nyekundu.
Chile haijawahi kushinda kombe la Copa kwa karibu karne moja. Chile wanaingia fainali hapo Jumamosi ambapo huenda wakachuana na Argentina au Paraguay.
No comments:
Post a Comment