Umoja wa Afrika umesema
hautawapeleka waangalizi wake wa uchaguzi katika uchaguzi wa wabunge wa
Burundi utakaofanyika Jumatatu kwa sababu masharti ya uchaguzi huru na
wa haki hayajazingatiwa.
Mapema Jumapili, Spika wa bunge la Burundi Pie Ntavyohanyuma alisema alikimbia nchi yake kwa sababu ya kuhofia usalama wa maisha yake baada ya kumshauri rais asigombee tena.
Jaribio la Bwana Nkurunziza kupata muhula wa tatu limekumbana na wimbi la ghasia ambapo zaidi ya watu sabini wameuawa.
No comments:
Post a Comment