WAZIRI wa kilimo, Chakula na Ushirika Steven Wasira amewafukuza kazi
wakurugenzi watendaji watatu wa Mamlaka ya Kuendeleza Bonde la Mto
Rufiji (Yaani Rufiji River Basin Development Authority – RUBADA)
kutokana na matumizi mabaya ya ofisi ya Umma ambayo yameitia hasara ya
Bilioni 2.5 Serikali .
Akitoa agizo hilo leo mbele ya Waandishi wa Habari, Waziri Wasira
amewataja Watendaji hao kuwa ni Bwana Aloyce L. Masanja – Kaimu
Mkurugenzi Mkuu; Bibi Tabu Ndatulu – Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji;
na Bwana Filozi John Mayayi – Mkurugenzi wa Fedha na Utawala.
Wassira amesema baada ya Ofisi yake kupata malalamiko kutoka kwa
wananchi wa vijiji vya Rufiji pamoja na wawekezaji juu ya Urasimu wa
shirika hilo, aliunda timu ya Uchunguzi kutoka wizara ya Kilimo na
Hazina kwenda kuchunguza malalamiko hayo.
“Baada ya kuunda tume kutoka hapa Wizarani ikishirkiana na Hazina,
walienda kwenye shirika hilo kufanya ukaguzi.Tume ilibaini kwamba
mfumo wa pale ulikuwa ni mbovu, wakurugenzi hawa walijifanya
wahasibu, wakawa wanakuanya pesa wenyewe na kutembea
nazo.Walifanya maksudi tu ili kujiwekea mianya ya kuiba Fedha”
Amesema Wassira
Taarifa ya Mheshimiwa Wasira imeanisha kuwa kati ya shilingi 2.748
billion zilizokuwa zimekusanywa kwa ajili uwekezaji, ni shlingi 714.606
milioni tu ndizo zimetumika kihalali wakati kiasi kilichobaki kimetumika
bila kuzingatia sheria na kanununi za fedha za umma.
Waziri Wassira amesema kuwa mbali ya kuiba pesa hizo, kamati ilibaini
kwamba watendaji hao wametumia zaidi ya Milioni 314 kwenye matumizi
yaliyo kinyume cha utaratibu
ikiwemo pesa zilizotengwa kwa ajili maendelea ya miradi ya Shirika hilo ambazo zimetumika ndivyo sivyo.
Vilevile Waziri Wassira amesema hata pesa ambazo wamewakata wafanyakazi
kwa ajili ya kupelekwa kwenye mifuko ya Hifadhi ya Jamii zimekuwa
zikiliwa na watendaji , tena kwa makusudi pasipo kupelekwa huko.
Aidha,Waziri Wasira amesema baada ya kupata Ripoti ya Tume hiyo
ameiagiza Bodi ya shirika la Ludaba kuwafukuza kazi mara moja watendaji
hao watatu na nafasi zako kujazwa mara moja huku taratibu na sheria za
kuwafikisha mahakamani zikifanyika.

No comments:
Post a Comment