Kwa mara nyingine tena, Uchina
imemlaumu kiongozi wa Tibet aliyeko uhamishoni Dalai Lama, kwa kutokuwa
mwaaminifu na kushinikiza kiujanja uhuru wa watu wa Tibet. China
inadai kuwa kiongozi huyo amebadilisha mbinu badala ya kutaka
kutambuliwa kwa jimbo hilo kama alivyokuwa akishinikiza hapo awali.
Uchina imemlaumu kiongozi wa Tibet aliyeko uhamishoni Dalai Lama, kwa kutokuwa mwaaminifu
China
imeanzisha makabiliano makali dhidi ya kiongozi wa kidini wa watu wa
Tibet, Dalai Lama, na kumlaumu kwa kutumia ghasia kushunikiza uhuru wa
Tibet. Katika taarifa ndefu inayoelezea mfumo mzima ya maoni ya jimbo la
Himalaya, China inasema kuwa katika hali ilivyo sasa, hakuna haja kabisa
ya kufanya mazungumzo na kinara huyo wa kidini aliye uhamishoni India.
China imeanzisha makabiliano makali dhidi ya kiongozi huyo wa kidini wa watu wa Tibet
Kwa
muda mrefu Dalai Lama amekuwa akitetea uhuru wa kujitenga wa jimbo la
Tibet, na alikuwa na matumaini makubwa kwa Rais wa sasa wa China, Xi
Jinping, atatumia mbinu tofauti katika uhusiano naye na wa watu wa
Tibet.
Taarifa hiyo pia ambayo ilichapishwa na shirika la habari
la kitaifa la Xinhua, inasema kuwa wakuu mjini Beijing wanamuomba Dalai
Lama kuweka kando ndoto yake ya hatma ya baadaye ya Tibet.
Aidha China inamtaka akubali kuwa jimbo hilo limekuwa sehemu ya China
kwa miaka na mikaka na kuwa hilo halitabadilika hivi karibuni.
Haijajulikana ni kwa nini taarifa hiyo ya kina imetolewa sasa.
Lakini
waandishi habari mjini Beijing wamejitokeza hivi majuzi na kupinga
maoni hayo ya Dalai Lama ambaye amekuwa uhamishoni nchini India tangu
mwaka 1959.
No comments:
Post a Comment