 |
| Kikosi
cha Wachezaji wa Zamani wa Timu ya Barcelona wakiwa katika picha ya
pamoja baada ya kuwasili Uwanja wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume
wakitokea Arusha. |
 |
| Rais wa Heshima wa Timu ya
Barcelona Kocha Johan Cruyff, akizungumza na waandishi wa habari wa
vyombo mbalimbali vilioko Zanzibar alipofika uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Abeid Amani Karume. |
 |
| Waandishi wa habari za michezo
Zanzibar wakiwa katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa kuipokea Timu ya
Wachezaji wa Wazamani wa Timu ya Barcelona |
 |
| Kikundi cha ngoma wakitowa burudani wakati wa ujio wa Wachezaji wa zamani wa timu ya Barcelona Zanzibar. |
 |
Viongozi wa vyama vya mpira
Zanzibar wakiwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wakiipokea timu ya
Wachezaji wa zamani wa Barcelona walipowasili Zanzibar.
|
 |
| Ndege ya Serikali ya Tanzania
ikiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume
ikiwa imewabeba wachezaji wa nyota wa Zamani wa timu ya Barcelona
wakiwasili Zanzibar. |
 |
| Mwenyekiti wa Baraza la Taifa
la Michezo Zanzibar Bi. Shery Khamis akisalimiana na mchezaji nyota wa
timu ya wachezaji wa zamani wa Barcelona Patrick Kluivert alipowasili
uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume. |
Wachezaji nyota wa timu ya
Barcelona wakisalimiana na viongozi wa vyama vya michezo Zanzibar baada
ya kuwasili katika uwanjani hapo.
 |
| Patrick Kluivert akitabasamu baada ya kushuka kwenye ndege. |
 |
| Patrick Kluivert akicheza na mmoja wa wanakikundi cha burudani uwanjani hapo. |
 |
Barcelona wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Zanzibar.
|
 |
Patrick Kluivert katika picha ya pamoja na waandishi wa habari wa Zanzibar.
|
 |
Barcelona wakipanda kwenye gari ili kuondoka kiwanjani hapo.
|
 |
| Kikundi cha ngoma wakitoa burudani. |
Magwiji wa soka wa timu ya zamani ya
Barcelona Hispania waliwasili visiwani jana Zanzibar kwa Mwaliko rasmi
wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, lengo kuu ikiwa ni kuitembelea Zanzibar
kujionea Vivutio vya Utalii na kujionea Vipaji vya Wachezaji Vijana
wanaocheza katika timu mbalimbali za Watoto.
Nyota hao wa zamani wa Barcelona watakuwa
dimbani leo jioni kukipiga na timu ya taifa ya zamani (Taifa Stars)
katika Uwanja wa Taifa.
No comments:
Post a Comment