Thursday, 9 April 2015

TEVEZ WA MASHAUZI AFANYA DUA

Mume wa ‘long time’ wa mwimbaji nyota wa kike wa muziki wa Taarab nchini, lsha Ramadhan ‘Mashauzi’, Jumanne Hassan ‘Tevez’ ambaye hivi karibuni alitekwa na kuteswa na watu wasiofahamika nchini Afrika Kusini, amerejea nchini na kufanya dua ya kumshukuru Mungu kwa kumnusuru kifo katika tukio hilo.
Tevez aliwakusanya ndugu, jamaa na marafiki na kufanya dua hiyo, Ijumaa iliyopita nyumbani kwao Msamvu, Madawa jirani na Shule ya Msingi Msamvu ‘A’

No comments:

Post a Comment