Friday, 10 April 2015

Somalia sasa yatoa orodha ya Al Shabaab

Serikali ya Somalia imetangaza ruzuku ya dola milioni moja kwa yeyote atakayeisaidia kuwakamata viongozi 11 wa Al Shabaab. Orodha hiyo ya watu 11 wanadaia kuwa viongozi wa ngazi ya juu ya katika kundi hilo la wapiganaji wa wa kiislamu wa Al shabaab.
Kiongozi wa kundi hilo la wapiganaji Ahmed Diriye anaongoza katika orodha hiyo huku Serikali ikitoa ruzuku ya dola laki mbili u nusu ($250,000) kwa yeyote atakayetoa habari zitakazofichua aliko.
 
Jumla ya dola milioni moja zimetengwa katika hatua hii ambayo inalenga kuchochea umma kuisaidia serikali hiyo kuitokomeza kundi hilo linalolaumiwa kwa mauaji ya zaidi ya wanafunzi 148 wa chuo kikuu cha Garissa nchini kenya.

No comments:

Post a Comment