Monday, 27 April 2015

Siku ya pili ya maandamano burundi

Wanaharakati wa upinzani nchini Burundi wanaandamana kwa siku ya pili wakipinga uamuzi wa kumtangaza Rais Pierre Nkurunziza kugombea nafasi ya urais kwa muhula wa tatu. Polisi walivunja maandamano kwa kutumia gesi ya kutoa machozi na maji ya kuwasha.

Watu wapatao watatu waliuawa katika ghasi hizo nchini Burundi Jumapili wakati polisi walipofyatua risasi za moto hewani kuwatawanya waandamanaji.

Maelfu ya watu wamepuuza amri ya kuwataka kutokwenda kuandaamana mitaani katika mji mkuu Bujumbura.
Awali alikitaka chama tawala kutomteua rais kuwania awamu ya tatu ya uongozi, akisema kufanya hivyo ni kukiuka katiba na mkataba wa amani wa Arusha.

Bwana Nkurunziza ametumikia nafasi ya urais kwa vipindi viwili, akiingia madarakani baada ya kumalizika kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Katiba ya Burundi inamruhusu rais kuchaguliwa mara mbili. Lakini wafuasi wa Bwana Nkurunziza wanasema anastahili kugombea kipindi kingine kwa kuwa alichaguliwa na bunge mwaka 2005.
Upinzani unasema hatua hiyo inatishia mpango wa amani ambao ulimaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka 2005 vilivyodumu kwa miaka 12.

No comments:

Post a Comment