Staa wa Bongo Movies, Shamsa Ford amemmwagia sifa Staa wa Bongo Fleva,
Nay wa Mitego kuwa hakuwahi kujua kama ni mkarimu huku akidai kuwa
anafaa kuwa mume!
Shamsa ambaye aliachana na mume wake tangu October mwaka jana, ameiambia
Bongo5 kuwa aliombwa na Nay ashirikishwe katika filamu yake.
“Sisi ni washkaji sema Nay ana kazi yake ya filamu ndio akaona mimi ndo nafaa, Hakuna kitu chochote zaidi ya kazi,” amesema Shamsa.
“Kabla ya kupata nafasi ya kuongea na Nay nilikuwa namuona ni mtu
fulani mgomvi mgomvi, in short nilikuwa simpendagi! Kama unakumbuka
aliwahi kutuponda Bongo Movie na mimi kuna siku nilihojiwa na kituo
kimoja nikamponda sana! Lakini nimekuja kukutana na Nay nimegundua ni
mtu tofauti sana. Sasa hivi mimi namzungumzia Emmanuel is man ambaye
kila mtu au kila mwanamke anaweza akamhitaji kuwa naye! Ana huruma ana
upendo, he is a good man, kama nilivyosema mwanamke yoyote atapenda kuwa
naye. Kwahiyo ni husband material,” aliongeza Shamsa.
Kwa upande mwingine, Shamsa amewataka mashabiki wa kazi zake kutambua
kuwa yeye ni mtu mzima na ana maamuzi ya kufanya kile anachokipenda ili
mradi asiharibu kazi.
“Mashabiki wangu wajue Shamsa mimi najielewa najitambua ni mkubwa na
ninajua zuri na baya,” amesisitiza muigizaji huyo. “Wasinihukumu kwa
ambacho wanakiona au wanachokisikia, wanisubiri mimi kama mimi Shamsa na
hayo wanayoyasikia hayawezi kuniharibia mimi kazi zangu au kuachana
mimi na mume wangu ndo nitashuka kisanii, hapana! Wasihukumu hivyo, mimi
nipo makini na kazi zangu.”

No comments:
Post a Comment