Raia wa Palestina wanasema kuwa
wamekubali kushirikiana na serikali ya Syria ili kujaribu kuwafurusha
wapiganaji wa IS nje ya kambi moja ya wakimbizi viungani mwa Damascus.
| Wakimbizi wa Palestina |
Wapiganaji wa IS walitekeleza shambulizi katika kambi hiyo wiki iliopita na kuweza kuiyumbisha kanbi hiyo licha ya pingamizi kutoka kwa jeshi la Palestina.
Takriban wakimbizi elfu kumi na nane wanaishi katika kambi hiyo ambayo inakabiliwa upungufu mkubwa wa vitu muhimu.
No comments:
Post a Comment