Monday, 13 April 2015

Nigeria:APC yatwaa majimbo19 kati ya 29

Chama cha rais mteule wa Nigeria APC, kimesajili ushindi mkubwa wa majimbo 19 kati ya 29 katika matokeo ya hivi punde yaliyotangazwa na tume huru ya uchaguzi INEC.
APC, kimeshinda majimbo makuu ya Lagos kaduna na Katsina katika uchaguzi mkuu wa Nigeria
Awali INEC ilikuwa imethibitisha kuwa chama cha rais mteule The All Progressives Congress (APC) kilikuwa kimetwaa miji mikuu ya Lagos Kaduna na na Katsina.
Matokeo haya ya hivi punde ni dhihirisho kuwa raia wa Nigeria walipigia Kura kiongozi wa upinzani Jenerali mtaafu Muhammadu Buhari.

Ushindi huo ni dhidirisho ya kuwa chama kinachoondoka madarakani cha Rais Goodluck Jonathan PDP kimepata kichapo chake kikubwa zaidi tangu kukamilika kwa utawala wa kijeshi mwaka wa 1999.
Jenerali mstaafu Muhammadu Buhari anatarajiwa kuapishwa rasmi kama rais wa taifa hilo lenye uchumi mkubwa zaidi barani Afrika mwishoni mwa mwezi Mei.
Mwandishi wa BBC aliyeko Abuja Bashir Saad Abdullahi anasema kuwa chama cha jenerali mstaafu Muhammadu Buhari The All Progressives Congress (APC)
Kilihifadhi jimbo la Lagos mbali na kutwaa majimbo zaidi ya Kaduna naKatsina.
Ushindi huu wa majimbo zaidi unaiongezea pondo serikali mpya haswa baada ya kutwaa ushindi mkubwa dhidi ya Rais Goodluck Jonathan.
Matokeo kamili ya kura za majimbo 39 na magavana 29 unatarajiwa kutolewa baadaye.
Jenerali mstaafu Muhammadu Buh

No comments:

Post a Comment