Mashirika ya kimataifa ya kutoa
misaada ya kibinadam, yameonya kuwa huenda yakalazimika kusitisha
shughuli zao zote nchini Somalia, ikiwa Kenya itabadili uamuzi wake wa
kufunga vituo vya kutuma na kubadilisha sarafu za kigeni maarufu kama
hawala, kufuatia shambulio lililofanywa na wapiganaji wa Al shabaab,
katika chuo kimoja kikuu mjini Garissa.
Kwa mujibu wa taarifa
kutoka kwa mashirika kumi na tano ya misaada, mashirika hayo hutumia
vituo hivyo kutuma pesa nchini Somalia na kulipa mishahara na kodi kwa
wafanyakazi wake.
Mashirika hayo yamesema, agizo hilo litakuwa na
athari kubwa sana kwa raia masikini wa Somalia, kwa sababu wao hutegemea
fedha wanazopokea kupitia vituo hivyo kununua chakula, kulipa karo na
pia kupata huduma za afya.
Serikali ya Kenya imesema imefunga
vituo hivyo ili kuzuia kundi hilo la Al shabaab kupokea fedha kutoka kwa
wafadhili wake katika mataifa ya kigeni.
No comments:
Post a Comment