Mawaziri wa mashauri ya kigeni wa
Ujerumani , Ufaransa , Urusi na Ukrain wameelezea wasi wasi uliopo
kufuatia kutokea kwa mapigano mashariki mwa ukrain na kikiukwa kwa
makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyoafikiwa mwezi Februari.
Baada
ya mazungumzo yaliyofanyika mjini Berlin waziri wa mashauri ya kigeni
wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier aliwaambia waandishi wa habari kuwa
kati ya silaha ambazo zitaondoa ni pamoja na vifaru.Pande hizo mbili zilionekana kuheshimu makubaliano hayo hadi kulipotokea mapigano ya hivi majuzi kwenye uwanja wa ndege wa Donetsk na kijiji cha Shyrokyne nje ya mji wa Mariupol.
Pande hizo pia zimekubaliana kuendelea kubadilishana wafungwa.
No comments:
Post a Comment