kocha wa timu ya taifa ya soka ya
wanawake nchini Tanzania ameomba kuandaliwa mechi za kirafiki za
kimataifa ili kujiandaa na fainali za Michezo ya Afrika (All Africa
Games) .
Rogasian Kaijage ameliomba shirikisho la mpira wa miguu
nchini Tanzania kufanya mipango ili wacheze na nchi kama Zimbabwe,
Afrika ya Kusini au Nigeria.Twiga imeitoa Zambia katika hatua za mchujo na sasa inajiandaa na safari ya Congo Brazzavile mwezi wa Septemba kwa michuano hiyo ya michezo ya Afrika, Twiga imefuzu kwa jumla ya mabao 6-5, kufuatia ushindi wake wa awali wa 4-2 ulioupata katika mechi ya kwanza iliyochezwa mjini Lusaka.
Michuano hiyo ya Michezo ya Afrika itashirikisha timu katika michezo mbalimbali, ikishirikisha timu za Afrika.
No comments:
Post a Comment