Rais wa chama cha wanariadha wa
kulipwa cha Kenya Wilson Kipsang amepinga vikali mpango wa chama cha
riadha cha Kenya kuwasimamia wanariadha ambao meneja wao wamesimamishwa
kwa muda wa miezi sita na chama hicho.
Mwenyekiti wa chama cha
riadha cha Kenya Isaiah Kiplagat ametangaza Federico Rosa wa Italia na
Gerald Vandeveen wa Uholanzi wamefungiwa kwa miezi sita wakishukiwa
kuhusika na dawa za kuongeza nguvu.Kiplagat anasema watafanya uchunguzi kwa miezi hiyo sita na endapo watapatikana na hatia watafungiwa.
Uamuzi huo unatokana na kashfa ya wanariadha wa Kenya kutumia dawa za kuongeza nguvu.
Kufikia sasa zaidi ya wanariadha 30 wa Kenya wamepatikana na hatia ya kutumia dawa hizi za kusisimua misuli akiwemo bingwa mara mbili wa Boston Marathon Rita Jeptoo ambaye amefungiwa mwa miaka miwili.
Kiplagat ameeleza kwa kipindi cha miezi hiyo sita ni chama hicho kitawakilisha wanariadha kama maajenti wao.
Lakini Kipsang ambaye pia ni bingwa wa Boston Marathon anasema hawatakubali kamwe kusimamiwa na chama hicho kwa sababu hawana imani nao kwa maswala ya fedha.
Kipsang amesema ni makosa kwa chama cha riadha nchini Kenya kufungia maneja wao bila kuwajulisha na kuwa na ushahidi wanahusika na madawa ya kuongeza nguvu.
No comments:
Post a Comment