Jaji mmoja na wakili ni miongoni mwa
watu waliouawa baada ya mshukiwa mmoja kuwafyatulia risasi ndani ya
mahakama moja mjini Milan nchini Italia. Maafisa wa idara ya
mahakama wanasema kuwa mshukiwa aliyefyatua risasi ni mtu mmoja
aliyekuwa akikabiliwa na kesi ya kutangazwa kufilisika.
Mshukiwa huyo aliwapiga risasi watu wawili ndani ya mahakama kabla ya
kumshambulia jaji ambaye angelisikiliza kesi yake ndani ya ofisi yake. Mtu wa nne anaaminika kufariki kutokana na mshtuko wa moyo.
No comments:
Post a Comment