Mshambuliaji wa timu ya Chelsea F.C. Didier Drogba amezindua
hospitali ya kwanza, kubwa na ya aina yake kati ya tano alizo wahi
kuahidi kuzijenga kama sehemu ya kujitolea kwa jamii yake .
Hospitali hiyo iko wilaya ya Attécoubé katika mji wa kibiashara wa
Abidjan, hospitali hiyo imemgharimu nguli huyo wa kandanda kiasi cha
dola milioni moja za kimarekani ili kukamilisha mjengo huo wa afya ;na
hospitali hiyo ni maalumu kwa wanawake na watoto wasio na uwezo wa
kumudu gharama za matibabu .
 |
| Mshambuliaji wa Chelsea Didier Drogba. |
Hospitali hiyo imejengwa katika eneo lenye ukubwa wa mita za mraba
mia nane (800) huduma kadhaa zinapatikana ikiwamo chumba cha uchunguzi,
wodi ya wazazi,kitengo cha watoto,jengo la x-ray ,jengo la kisasa la
maabara,duka kubwa la dawa,jengo la kulaza wagonjwa na jengo tengefu la
wagonjwa.

Inakadiriwa
hospitali hiyo itakuwa na uwezo wa kuhudumia wagonjwa elfu hamsini kwa
mwaka na hii ni kwa muujibu wa katibu mkuu wa asasi ya Didier Drogba
Foundation , Guy Roland Tanoh ambaye ndiye msimamizi mkuu wa mradi huo.
Hospitali zingine nne zilizo katika ahadi za mwanasoka huyo ziko
katika hatua za ujenzi za mwisho mwisho kukamilika ambazo ziko nchini
Ivory Coast katika miji ya Yamoussoukro, San Pedro, Man na Korhogo na
zinatarajiwa kuzinduliwa rasmi mwezi ujao.
Asasi hiyo ya Drogba foundation inaandaa chakula cha hisani mjini
London mwezi huu wa April tarehe 18 ili kupata fedha za kukamilisha
miradi hiyo.
Mshambuliaji huyo wa timu ya Chelsea na pia timu ya Elephants
anabakia kuwa mchezaji na mfungaji bora na wa mfano wa kuigwa nchini
mwake pamoja na kwamba amestaafu kuichezea timu yake ya taifa,ambayo
iliutwaa ubingwa wa kombe la mataifa ya Africa mwaka huu nchini
Equatorial Guinea mnamo mwezi wa February.Kazi nzuri Didier Drogba! .
No comments:
Post a Comment