Shirikisho la mpira wa miguu duniani
(FIFA) limetoa viwango vipya vya soka duniani huku Tanzania na Rwanda
zikishuka kwa nchi za Afrika ya Mashariki wakati Kenya, Uganda na
Burundi zikipanda viwango.
Uganda ndio nchi inayoongoza katika Afrika ya Mashariki ikipanda nafasi mbili juu na kushika nafasi ya 72 baada ya kuwafunga Nigeria 1-0.
Burundi nayo imepanda kutoka nafasi ya 126 mpaka ya 123 mbali ya kutoka droo ya 2-2 na timu ya Mauritius.Kenya pia imepanda nafasi moja juu na sasa ipo ya 117 huku ikiwa na rekodi ya kuifunga Shelisheli 2-0 katika mechi yake ya kirafiki.
Mbali na Afrika ya Mashariki, kiujumla kumekuwa na mabadiliko makubwa katika viwango hivyo vya mwezi April.
Miongoni mwa nchi zilizopanda ni Belgium ikiwa ya tatu baada ya kupanda juu nafasi moja kufuatia ushindi wake katika michuano ya Ulaya ya EUFA. Brazil pia ni miongoni mwa nchi zilizopanda, ikiwa ya ya 5, ikipanda nafasi 1.
1. Ujerumani
2. Argentina
3. Belgium
4. Colombia
5. Brazil
6. Netherlands
7. Portugal
8. Uruguay
9. Swizerland
10. Uhispania
No comments:
Post a Comment