Tovuti hiyo itakuwa na kiwambo kwa kikubwa (full-screen)
itakayoonyesha mawasiliano ya watumiaji na itamwezesha mtumiaji kuweka
dondoo (notifications) mbalimbali na kuweza kuzima kwa muda mawasiliano.
Kama ilivyokuwa awali katika huduma ya Messenger kwenye Facebook.com,
mtumiaji ataweza kutuma picha, stika kwa watu wake kupitia
Messenger.com. Unapoingia katika tovuti hiyo kwa kutumia taarifa zako za Facebook,
Messenger.com inakusanya meseji zako za karibuni na inazionyesha katika
kiwambo kwa ukubwa (full-screen).
Hapo mtumiaji ataweza kupiga simu au kuchati kwa kutumia video (video
chats) kupitia menyu zilizopo juu mkono wa kulia na kwa upande wa
kushoto mtumiaji ataweza kupunguza au kuongeza sauti, kuona dondoo
mbalimbali na kuweza kumzuia mtumiaji mwingine.
Messenger.com kwa sasa inapatikana kwa lugha ya Kiingereza, ila
Facebook itaongeza huduma ya lugha nyingine karibuni. Mbali na hilo,
tovuti mama ya Facebook itaendelea kuwa na huduma yake ya Messenger kama
zamani.
Huduma ya Facebook Messenger inatumiwa na watu zaidi ya milioni 600
kwa mwezi. Kwa ujumla mtandao wa Facebook unatembelewa na takribani watu
bilioni 1.4 kwa mwezi huku watu takribani milioni 890 wakitembelea
Facebook na kutazama zaidi ya video bilioni tatu kwa siku.
Mwaka uliopita, Facebook walinunua mtandao wa WhatsApp kwa Dola za
Kimarekani bilioni 19. Mwaka huu WhatsApp walizindua huduma yao kupitia
kwenye kompyuta ambayo inamuonekano kama wa Messenger.com.
Kwa sasa WhatsApp inayo huduma ya kupiga simu kupitia simu za Android
na katika wiki za karibuni itazindua huduma hiyo katika simu
zinazotumia iOS.
No comments:
Post a Comment