Shirika la afya duniani WHO limesema kuwa Ebola bado imebaki kuwa janga la kimataifa.
Takwimu za hivi majuzi zinaonyesha kuwa kuwa ni visa vipya 30 vya ugonjwa wa Ebola vilivyothibitishwa nchini Guinea na Sierra Leone ikilinganishwa na mamia ya visa hivyo siku za nyuma.
WHO inasema kuwa ugonjwa wa Ebola uliwaua karibu watu 10,600 katika mataifa hayo ya Magharibi mwa Afrika.
Aidha WHO inasema kuwa jamii ya kimataifa inapaswa kuweka tahadhari kuu dhidi ya mlipuko huu ama mwengine wa Ebola.
No comments:
Post a Comment