Waziri wa masuala ya ndani nchini
Afrika kusini ametoa wito kwa viongozi wa kitamaduni kukoma kutoa
matamshi yasiyo na msingi ambayo yanaweza kusababisha maafa.
Waziri
Malusi Gigaba amesema hayo baada ya mfalme wa Kizulu, Goodwill
Zwelithini kusema kuwa wahamiaji wanapaswa kufunga virago vyao na
kuondoka nchini humo.
waziri wa maswala ya ndani nchini Afrika kusini malusi Gigaba
Idara ya polisi nchini humo imesema kuwa zaidi ya wahamiaji elfu moja
wameondoka kutoka mji wa mashariki mwa Durban katika kipindi cha siku
chache zilizopita, kwa hofu ya kushambuliwa na raia wa nchi hiyo. Raia wa kigeni hushambuliwa mara kwa mara nchini Afrika Kusini.
No comments:
Post a Comment